Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ammouta achukua Mikoba ya Da Cruz FAR Rabat

Houcine Ammouta Ammouta achukua Mikoba ya Da Cruz FAR Rabat

Mon, 29 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya FAR Rabat ya Morocco imemteua mkufunzi Houcine Ammouta kuwa kocha mkuu klabuni hapo kuchukua mikoba ya Fernando Da Cruz aliyefutwa kazi. Ammouta (53) raia wa Morocco amewahi kuvinoa vilabu vya Wydad Casablanca na FUS Rabat .

Ammouta aliiongoza Wydad Casablanca kutwaa Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2016/17 huku akitwaa ubingwa wa Ligi kuu Morocco ya Botola Pro 2016/17 sambamba na kuchaguliwa kuwa kocha bora wa msimu wa 2016/17.

Mnamo 2010 Ammouta akiwa kocha FUS Rabat aliiongoza klabu hiyo kutwaa kombe la mfalme Morocco sambamba na kombe la Shirikisho Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live