Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Amiss Tambwe kwenye benchi la Ufundi Aigle Noir

Amisi Tambwe Amiss Tambwe

Fri, 19 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kufanya vyema akiwa na timu za Yanga SC na Simba SC, Mchezaji wa zamani wa Kimataifa wa timu ya taifa ya Burundi ‘Intamba Murugamba’ Amiss Tambwe atakuwa miongoni mwa wanaounda benchi la ufundi la Klabu ya Aigle Noir inayoshiriki Ligi Kuu nchini Burundi.

Amiss Tambwe anarejea katika klabu yake ya awali ya Aigle Noir iliyoibua kipaji chake ambapo aliitumikia mwaka mmoja wa 2008-2009 kabla ya kutimkia katika timu ya Vital’O na kuitumikia kuanzia 2010-2013.

Baada ya kugeukia masuala ya ukocha Amiss Tambwe ataweza kuhudumu chini ya kocha Jimmy Ndayizeye, kocha wa Messager Ngozi kwa msimu uliopita.

Aigle Noir ambayo haikumaliza kwenye nafasi nzuri msimu uliopita inatarajia kuweka kambi siku kumi na nane jijini Dar es salaam katika kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Burundi 2024/2025.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live