Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Amiss Tambwe akiri anapitia magumu

Amissi Tambwe Amiss Tambwe akiri anapitia magumu

Mon, 5 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Mshambuliaji wa Singida Big Stars, Amissi Tambwe ameweka wazi kupitia changamoto kwenye timu yake hasa ya kutopata nafasi ya kucheza mara kwa mara kutokana na ushindani mkali uliopo kutoka kwa mastaa wenzake.

Kauli ya Tambwe inajiri baada ya nyota huyo kufunga bao lake la kwanza msimu huu akiwa na timu hiyo wakati kikosi chake kiliposhinda mabao 3-0 dhidi ya Namungo juzi, mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Liti Singida.

“Bao nililofunga limenirudisha kwenye hali yangu ya kujiamini kwa sababu kama mchezaji usipopata nafasi ya kucheza mara kwa mara lazima ujisikie vibaya lakini kikubwa ni kuangalia matokeo mazuri ya timu,” alisema.

Tambwe aliongeza licha ya kutokea benchi kwenye michezo mingi ila atahakikisha kila anapoingia uwanjani anatimiza majukumu aliyoagizwa kwani hiyo ndiyo njia nzuri ya kulishawishi benchi la ufundi kumtumia.

“Timu yetu ina wachezaji wengi na wazuri na ukiwa Professional (mchezaji wa kulipwa), lazima uheshimu uwezo wa wenzako na kuangalia ni kitu gani amekuzidi ili ukifanyie kazi na uwe bora zaidi yake,” alisema Tambwe.

Kwa upande wa kocha msaidizi wa timu hiyo, Mathias Lule alisema hakuna mchezaji ambaye ana uhakika wa namba kwenye kikosi chao isipokuwa wanafanya machaguo kutokana na ubora wa mpinzani wanayecheza naye siku husika.

Tambwe alifunga bao la tatu wakati akitokea benchi alipochukua nafasi ya Frank Zakaria huku mabao mengine yakifungwa na Said Ndemla ambaye naye ni bao lake la kwanza msimu huu pamoja na Meddie Kagere akifunga pia bao lake la nne.

Chanzo: Mwanaspoti