Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ambundo ashusha ujumbe mzito kuwaaga Yanga

Ambundo Ashusha Ujumbe Mzito Wa Kuwaaga Yanga Ambundo ashusha ujumbe mzito kuwaaga Yanga

Wed, 21 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa winga wa Yanga Sc, Dickson Ambundo, amewaaga Wananchi kwa kuandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Ujumbe hup ameuandika leo Juni 21, 2023 mara baada ya kupewa 'thank you' hapo jana na klabu yake hiyo kumtakia kila lakheri baada ya mkataba wake kumalizika na Yanga kutoonesha nia ya kuendelea naye.

"Moja kati ya nyumba bora sana, nyumba yenye upendo, furaha, matumaini na umoja wa hali ya juu, nyumba ya mafunzo yanayo toa mwanga mzuri kwenye safari ya maisha, kwa uzuni leo nawaaga wenzangu kwenye nyumba lakini moyo wangu umejawa na shukran za dhati kabisa kwa wenye nyumba kuanzia Uongozi bora kabisa chini ya rais @caamil_88 benchi la ufundi chini ya @nabi, wachezaji wenzangu na wananchi wote kwa ujumla. Mungu aendelee kuwabariki kuleta mafanikio zaidi katika safari yenu. Siku moja tutaonana tena nyumbani. Daima Mbele, nyuma mwiko.#Wananchi," aliandika Aambundo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live