Mfungaji wa bao la ushindi kwa upande wa Yanga, Dikson Ambundo amekiri kuwa amepoteza nafasi nyingi za wazi lakini amefunga bao la ushindi ambalo lilikuwa kwenye mazingira ambayo hakuyatarajia.
Ambundo aliifungia timu yake ya Yanga bao la ushindi dakika 90 za mchezo dhidi ya KMKM baada ya kuunganisha kwa kichwa mpira uliochongwa na Bakari Mwamnyeto.
Anasema amesahau nafasi nyingi za wazi alizozipoteza na kusawazisha makosa kwa kugunga bao katikati ya msitu wa mabeki wa KMKM.
“Nimefunga bao katika mazingira magumu ambayo sikutarajia kama mpira utanifikia nilikuwa katikati ya mabeki wa timu pinzani mpira wa juu ulipigwa na nahodha nikaruka na kuukandamiza ndani ya nyavu,” alisema na kuongeza;
“Nimecheza vizuri lakini nimeshindwa kufikia asilimia mia za maelekezo ya kocha kutokana na kukosa nafasi nyingi japo nimefunga na kuipa matokeo timu najipanga kurudi uwanja wa mazoezi kurekebisha makosa yangu tayari kwa mchezo unaofuata ambao ni mgumu zaidi.”
Ambundo anasema wanamzo mgumu dhidi ya Singida Big Stars Ijumaa wanajiandaa kupambana kwa lengo la kuhakikisha wanatinga hatua ya nusu fainali.