Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ambulance yasimamisha mechi ya Namungo vs Mbeya City

FC Namungo.jpeg Namungo FC

Fri, 13 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MCHEZO kati ya Namungo FC dhidi ya Mbeya Kwanza ambao ulitarajiwa kuchezwa leo Mei 13 umesimamishwa na haujachezwa kutokana na kutokuwepo kwa gari ya wagonjwa.

Kabla ya mchezo huo uliotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Ilulu,hakukuwepo na gari ya kubebea wagonjwa, (Ambulance).

Hata hivyo muda ambao waliweza kukaa kwa kusubiri gari la wagonjwa kwa muda wa dk 15 hakukuwa na gari la wagonjwa.

Pia mpaka dk ya 20 inafika hakukuwa na gari la wagonjwa ambapo inaelezwa kuwa gari lilikuwepo lakini liliweza kuondoka kwa kupata dharula.

Baada ya mgomo huo gari la wagonjwa likaletwa saa 10:23 jioni wakati mechi ilikuwa ianze saa 10:00 jioni, Timu zimeondoka uwanjani na sasa yanasubiriwa maamuzi ya Mamlaka za Soka nchini.

Taarifa zaidi endelea kufuatilia TanzaniaWeb.com

Chanzo: www.tanzaniaweb.live