Bao pekee lililofungwa na Mudathir Yahya katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Namungo FC limeifanya Yanga SC kuongoza katika msimamo wa ligi hiyo wakifikisha pointi tisa.
Mudathir amefunga bao hilo dakika ya 88, baada ya kuingia kipindi cha pili kuchukuwa nafasi ya Pacome Zouzoua.
Baada ya mchezo huo kumalizika, huu ni uchambuzi wa George Ambangile wa Wasafi FM;
THIRD MAN RUNNER .
Kuna silaha kadhaa za kutumia pale unapokabiliana na timu ambazo zinakabia chini sana (Low block) niliwahi kuzianisha hapa siku ambayo Arsenal walicheza Vs Everton majuzi, ngoja nizitaje tena.
1: Vuta subira usifosi mambo ukiwa na mali
2: Tanua uwanja pembeni zaidi kwa matumizi ya wingers
3: A Third Man Runner + Cutbacks ( yule mchezaji wa tatu anayeshambulia space iliyowazi wakati wenzake wawili wanapasiana )
4: Piga mashuti sana ( Ball striking )
5: Dumisha muundo wako wa ulinzi pale unapokuwa na mpira ( rest defense ) ili kuepuka madhara ya counter attacks kutoka kwa mpinzani wako lakini pia kudumisha mashambulizi.
Kati ya hizo 5 unaona ipi imetumika kuifungua Namungo kutoka kwa Yanga SC
2, 3 na 5 ✅
Goli la Mudathir ni kuwa a third man runner wakati wenzake wawili wanapasiana (Aziz Ki na Yao) wakati Jesus Moloko aliingia kufanya uwanja kuwa mpana zaidi kama winga halisi huku Job, Bacca na Aucho walikuwa na muundo mzuri wa ulinzi pale Yanga wakiwa na mpira ili kukabiliana na Buswita Kichuya kwenye counter attacks lakini wakianzisha mashambulizi haraka pale Yanga wakirudisha mpira kwenye himaya yao.
Plan ya Cedric Kaze ilikuwa nzuri kulingana na alichokuwa anatafuta kwenye mechi ya leo.
1: Kuzuia kwa idadi kubwa ya wachezaji wakiwa karibu karibu sana why?
2: Kufunga space baina ya mstari mmoja na mwingine lakini pia baina ya mchezaji na mchezaji ili kuwalazimisha viungo wabunifu wa Yanga kukosa nafasi ya kufanya yao.
3: Kusubiri Counter attacks kama njia ya kupata goli
3-4-3 wakiwa na mali na 5-4-1 bila mpira (Nyoni Mukombozi na Asante) ni perfect kabisa kwa muundo wa Back 3, wote wapo comfortable sana wakiwa na mali mguuni hawapaniki wakati Nyenye na Domayo wanakupa energy na ulinzi mbele yao.
Kilichokosekana kwa Namungo ni kushambulia kwa idadi kubwa ya wachezaji pale wakiwa na mpira.
NOTE
1: Kuna nyakati kadhaa uchaguzi wa umaliziaji ndio uliwaangusha Yanga (Maxi, Aziz Ki, Pacome).
2: Sijui kama Kaze ataendelea na huu muundo, nafikiri ni mzuri sana inachotakiwa ni kuboresha kwenda mbele.
3: Mechi 3 ushindi 3 na clean-sheets 3 magoli 11 ya kufunga : Yanga hao.