Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alvarez sasa aingia anga za Atletico Madrid na PSG

Image 11b2393d B04f 4993 8e9e 8a3a19524490 85 2560 1440.jpeg Alvarez sasa aingia anga za Atletico Madrid na PSG

Fri, 19 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabosi wa Atletico Madrid wanahitaji huduma ya straika wa Manchester City na Argentina, Julian Alvarez, 24, katika dirisha hili kwa ajili ya kuziba pengo la mshambuliaji wao Alvaro Morata anayetarajiwa kujiunga na AC Milan katika siku chache zijazo.

Alvarez mwenye umri wa miaka 24, amekuwa akihusishwa na timu nyingi barani Ulaya tangu kuanza kwa dirisha hili na mbali ya Atletico, matajiri wa Jiji la Paris, PSG pia wanataka kumsajili.

Inaelezwa staa huyu amewaambia mabosi wa Man City kwamba anataka kuondoka katika dirisha hili kwa ajili ya kutafuta timu itakayompa nafasi kubwa zaidi ya kucheza.

Kabla ya kuwaambia kwamba anahitaji kuondoka, mabosi wa Man City walimwekea mezani ofa ya kusaini mkataba mpya lakini staa huyo alikataa.

Mkataba wa sasa wa Alvarez unatarajiwa kumalizika mwaka 2028. Msimu uliopita alicheza mechi 58 za michuano yote na kufunga mabao 19.

Staa huyu amekuwa akipata mafanikio makubwa kwa kushinda karibu kila kombe, licha ya kwamba hana namba ya kudumu.

KIUNGO wa Everton na Ubelgiji, Amadou Onana, 22, anatarajiwa kukamilisha uhamisho wake wa kujiunga na Aston Villa wikiendi hii.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Skysports, Onana atafanya vipimo vya afya ndani ya siku mbili zijazo na kama mambo yataenda sawa atasaini rasmi kuwatumikia vijana hao wa Unai Emery. Onana alijiunga na Everton kwa mkataba wa miaka mitano Agosti 9, 2022 kwa ada ya uhamisho ya Pauni 33 milioni.

AL-NASSR inaangalia uwezekano wa kumpata kipa wa Juventus na Poland, Wojciech Szczesny, 34, baada ya kuikosa huduma ya kipa wa Manchester City, Ederson. Matajiri hao wa Uarabuni wamekuwa katika msako wa kipa kwa muda mrefu na walianza na David de Gea, Allison Becker na baadaye Ederson lakini kote huko waliangukia pua, hivyo wameamua kujitosa kwa zWojciech ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2025.

VIGOGO wa Paris St-Germain wanadaiwa kuendelea na mazungumzo kwa ajili ya kumpata straika wa Napoli, Victor Osimhen, 25, katika dirisha hili ambapo timu yake ipo tayari kumuuza.

Osimhen ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika 2026, alikuwa akitajwa kuwa katika rada za Chelsea lakini kuingia kwa PSG inayotafuta mbadala wa Kylian Mbappe inaweza kuwaondoa kwenye mchakato huo.

DILI la beki wa Bayern Munich, Matthijs de Ligt kutua Manchester United huenda likafeli baada ya mashetani wekundu kuwa katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wa beki wa Lille, Leny Yoro.

Kusajiliwa kwa Yoro kutasababisha United itumie kiasi kikubwa cha pesa hivyo itashindwa kufikia kiwango cha Pauni 43 milioni kinachohitajika na Bayern ili kumuuza De Ligt.

De Ligt mwenyewe ndio amekuwa akilazimisha kuondoka kwa sababu anataka kuungana tena na kocha wake wa zamani Erik ten Hag anayeamini atampa nafasi zaidi.

IMEFICHUKA kuwa Aston Villa imeendelea kushikilia msimamo wa kuhitaji Pauni 60 milioni kutoka kwa Al-Ittihad ili kumuuza winga Moussa Diaby katika dirisha hili kwa sababu bado inadaiwa pesa za usajili na Bayer Leverkusen ambayo ndio iliwauzia staa huyo katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana kwa ada ya Euro 55 milioni.

Tovuti ya Football Insider imeripoti kwamba Villa inadaiwa nusu ya pesa hiyo.

Steven ambaye msimu uliopita alicheza mechi 31 za michuano yote na kufunga mabao 13, mkataba wake unamalizika mwaka 2027.

Awali Joshua mwenye umri wa miaka 23, pia alishafanya makubaliano na AC Milan.

WEST Ham ndio inaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kumsajili mshambuliajo wa Arsenal, Reiss Nelson, 24, ambapo imepanga kutumia Pauni 25 milioni ili kukamilisha dili hilo. Timu mbalimbali za EPL pia zilionyesha nia ya kutaka kumsajili staa huyu lakini ameonyesha kupendezwa zaidi na ofa na mipango ya West Ham.

WEST Ham imeanza mazungumzo na wawakilishi wa Ajax kwa ajili ya kuipata saini ya winga wa Ajax na Uholanzi, Steven Bergwijn, 26, na inataka kuwasilisha ofa kwa ajili ya kumsajili katika dirisha hili lakini kuna upinzani mkubwa kutoka kwa Marseille na timu mbili kutoka Saudi Arabia ambazo zinahitaji huduma yake pia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live