Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alvarez Julian: Tumefika tulipopataka

Julian Alvarez 4 Scaled E1633530306551 Alvarez Julian

Tue, 2 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kikosi cha Manchester City kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Fulham Juzi Jumapili (Aprili 30), Mshambuliaji kutoka nchini Argentina Alvarez Julian amekiri kuwa kwa sasa kila mchezo waliobakiza ni kama fainali.

Man City ilipata ushindi huo katika mchezo wa Ligi Kuu ya England uliochezwa Uwanja wa Craven Cottage, London nchini England.

Mabao ya Man City yaliwekwa kimiani na Erling Haaland na Alvarez wakati Carlos Vinicius aliifungia Fulham.

Kutokana na ushindi huo, Man City inaongoza msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 76 katika michezo 32 iliyocheza msimu huu.

Akizungumza katika tovuti ya Man City Muargentina huyo amesema kila mchezo kwao ni fainali na wanahitajika kuendelea kuongeza juhudi ili kupata matokeo mazuri.

“Hapa ni pale tulipotaka kuwa mwanzoni mwa msimu, kila mmoja anafanya kazi nzuri sana na sasa tumefikan kileleni, tunahitaji kulinda. Kila mchezo ni fainali kwetu,” amesema.

Katika ligi hiyo, Man City imebakisha michezo sita dhidi ya dhidi ya West Ham, Leeds, Everton, Chelsea, Brighton na Brentford.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live