Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alvarez, Guardiola vita ni kali

Guardiola Le Manager Repond Aux Derniers Commentaires De Julian Alvarez Sur Son Depart Alvarez, Guardiola vita ni kali

Fri, 2 Aug 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Straika wa Manchester City, Julian Alvarez amesisitiza hakusema chochote kibaya baada ya kocha wake Pep Guardiola kutoa jibu lililoashiria kutofurahishwa na majibu yake alipoulizwa juu ya hatma ya staa huyo.

Alvarez ambaye kwa sasa anaitumikia Argentina katika Michezo ya Olimpiki huko Paris, hivi karibuni alisema ataamua juu ya hatma yake pale atakapomaliza majukumu ya kuitumikia Argentina katika Olimpiki.

Moja ya mambo aliyoyasema katika mahojiano yake hayo ni hapendezwi na kitendo cha kuwekwa nje ama kuingizwa akitokea benchi katika michezo mikubwa.

Kwa msimu uliopita Alvarez alikuwa ndiye mchezaji aliyecheza mechi nyingi zaidi akiwa na wastani wa kucheza dakika tano zaidi kuliko nyota yeyote Man City.

Hata hivyo, mechi hizo nyingi ni zile ambazo hazikuonekana kuwa na umuhimu sana wakati zile zenye umuhimu kama fainali ya FA dhidi ya Manchester United hupangwa Erling Haaland.

"Msimu uliopita, nilikuwa mmoja wa wachezaji waliokuwa na dakika nyingi zaidi Man City, hakuna mchezaji anayependwa kuachwa nje katika mechi muhimu, lazima ahitaji kuchangia, nitafikiria hatma yangu baada ya Olimpiki na nitakuwa na mapumziko ya muda mfupi kisha nitaamua."

Baada ya kusambaa kwa mahojiano yake haya, waandishi walimuuliza Guardiola juu ya hatma ya staa huyu na kocha huyo akasema ameona mchezaji huyo alichokisema.

"Najua alichokisema, anataka kufikiria kuhusu mustakabali wake, atakapomaliza kufikiri wakala wake atampigia simu mkurugenzi wetu wa michezo na tutaona kitakachotokea. Nafahamu anataka kucheza katika mechi muhimu, ndiyo lakini kuna wachezaji wengine pia wanataka kucheza, tuna wachezaji 18 hadi 19 nao wanataka kucheza mechi kubwa, nimesoma alichokizungumza, mwache afikirie baada ya hapo atuambie nini anahitaji kufanya."

Kwa upande wa Alvarez naye alipoulizwa juu ya majibu hayo ya Guardiola alisema, hakuwa na nia mbaya wala sio kama hana furaha ya kucheza Man City, binafsi amekuwa na kawaida ya kujitathmini kila baada ya msimu kumalizika.

"Nilisikia alichosema Guardiola. Sina mengi ya kusema kuhusu hilo, sijawahi kusema chochote kibaya. Nilisema tu nitafikiria juu ya hatma yangu kama ninavyofanya kila msimu, huwa nafanya uchambuzi wa kile kilichotokea msimu uliopita na makadirio ya kile kinachoweza kutokea. Siku zote nasema ninajisikia furaha nikiwa Man City, ambayo ni timu kubwa. Kwa hiyo sikusema lolote baya."

Man City ilimsajili Alvarez kutoka River Plate, Januari 2022 kwa dau la Pauni 14 milioni lakini ikamrudisha kwa mkopo hapo hadi msimu ulipomalizika.

Chanzo: Mwanaspoti