Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alphonse Munyantwali Rais mpya wa Shirikisho la Soka Rwanda

IMG 4464 Alphonse Munyantwali.jpeg Alphonse Munyantwali

Mon, 26 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la soka Nchini Rwanda (FERWAFA) limemchagua Alphonse Munyantwali kuwa rais wake katika uchaguzi uliofanyika juzi Juni 24, 2023 katika Mkutano Mkuu wa FERWAFA.

Munyantwali ambaye alikuwa Mwenyekiti wa klabu ya Police FC kwa siku 58, anachukua mikoba ya Olivier Mugabo Niyezimana aliyejiuzulu mnamo Aprili na ataiongoza FERWAFA kwa miaka miwili ijayo.

FERWAFA ilichagua viongozi wapya baada ya Kamati ya Utendaji iliyoongozwa na Nizeyimana kuvunjwa kwa sababu wanachama wake wengi walijiuzulu na hivyo kuacha chini ya 2/3 yao kufanya uamuzi.

Kamati ya Utendaji inayoongozwa na Munyantwali, itasimamia miaka miwili iliyosalia ya muhula wa miaka minne wa uongozi wa Nizeimana Olivier, ambaye alijiuzulu mnamo Aprili 19, 2023.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live