Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alonso anakwenda Real Madrid baada ya Liverkusen

Xabi Alonso .jpeg Kocha wa Bayern Liverkusen, Xabi Alonso

Tue, 16 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Afisa mtendaji mkuu wa Bayer Leverkusen Fernando Carro, ameweka wazi kuwa siku moja kocha wao Xabi Alonso atakuwa kocha wa klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania.

"Ni wazi kuwa Xabi Alonso atakuwa kocha wa Real Madrid siku moja."

"Klabu nyingi zinamtaka Xabi, labda siku moja itawezekana lakini kwa sasa ana furaha kubaki na sisi."

"Kuhusu pesa ya kuvunja mkataba wake kwetu ni siri kati yetu".

- Fernando Carro Afisa Mtendaji mkuu wa Bayer Leverkusen, kuhusu kocha wake Xabi Alonso.

Alonso amepata umaarufu mkubwa baada ya kuipa ubingwa klabu ya Bayer Leverkusen bila kupoteza mchezo wowote wa Ligi huku kimataifa akiwa kwenye kiwango bora hajapoteza mchezo wowote na timu yake ikiwa katika hatua ya robo fainali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live