Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alonso anahitaji moja tu

Xabi Alonso .jpeg Kocha wa Bayern Liverkusen, Xabi Alonso

Mon, 8 Apr 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Muda wa kunyanyua makwapa kwa nahodha wa Bayer Leverkusen, Lukas Hradecky umewadia rasmi, kwani wanahitaji kushinda mechi moja tu ili kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Ujerumani ikiwa ni kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo iliyoanzishwa miaka 120 iliyopita.

Leverkusen wanahitaji kushinda mechi moja tu baada ya wapinzani wao wa karibu katika mbio za ubingwa Bayern Munich wikiendi iliyopita kupoteza mbele ya Heidenheim kwa kichapo cha mabao 3-2.

Wakati Bayern inapoteza, Leverkusen ilikuwa inapata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Union Berlin.

Kiujumla Leverkusen ina alama 76 wakati Bayern ina 60, hivyo katika michezo sita iliyosalia kabla ya ligi hiyo kumalizika ikiwa Munich itashinda yote itakuwa imefikisha pointi 78.

Hiyo inamaanisha kwamba ikiwa Leverkusen itashinda mchezo mmoja tu kati ya sita iliyobakia itafikisha pointi 79.

Mchezo ujao ambao Leverkusen inaelekeza nguvu zake zote ili kushinda na kutawazwa kuwa mabingwa ni wa nyumbani BayArena dhidi ya Werder Bremen ambayo inashika nafasi ya 11 ikiwa na alama 31.

Munich ipo kwenye hatari ya kupoteza ubingwa wa Bundesliga kwa mara ya kwanza baada ya kuchukua kwa misimu 11 mfululizo.

Mbali ya kufanya vizuri katika Ligi Kuu, vijana hawa Xabi Alonso pia wamekuwa bora katika michuano ya kimataifa ambapo kwa sasa wapo hatua ya robo fainali ya Europa League na watakutana na West Ham.

Chanzo: Mwanaspoti