Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ally Salim atoa kauli nzito Simba,

Ally Salim Simba Ally Salim

Sun, 7 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kipa wa Simba Ally Salim amesema ni bahati kwake kuona amepata nafasi ya kuitumikia Simba kwenye michezo ya Ligi Kuu Bara msimu huu, huku akisema anatakiwa kuongeza umakini.

Salim amefanikiwa kudaka michezo kadhaa muhimu ya Simba ya hivi karibuni kutokana na kipa namba moja wa timu hiyo, Aishi Manula kuwa na majeraha na kocha wa timu hiyo, Robert Oliviera Robertinho kuamua kumtumia yeye badala ya Beno Kakolanya ambaye alikuwa kipa namba mbili.

Akizungumza na Mwanaspoti, Salim alikiri ni bahati kupata nafasi hiyo, iliyokuwa adimu kwake kwa miaka mingi, ila funzo kubwa alilolipata ni kuongeza nidhamu kuanzia mazoezi hadi wakati wa mechi, kujiamini na kusikiliza zaidi maelekezo ya kocha wake.

"Simba ni timu kubwa yenye maono makubwa, ukifanya vibaya unaumiza mioyo ya watu, ukifanya vizuri unaleta utulivu na amani za mashabiki, haikuwa rahisi kwangu ila nashukuru Mungi nilipata usaidizi wa kutosha kuhakikisha nasimama kuisaidia timu.

"Jambo kubwa zaidi nililojifunza kwenye mechi nilizocheza ni kuongeza umakini dakika zote 90, kwani kila timu inakuwa na lengo la kutikisa nyavu ili kupata hitaji lake," alisema. Ikumbukwe michezo ambayo amefanikiwa kudaka kipa huyo ni dhidi ya Ihefu, Yanga, Wydad na Namungo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live