Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ally Salim afunguka nyuma ya pazia penati ya Kagere

Ally Salim Penatiiii.jpeg Ally Salim.

Thu, 11 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Simba imefanikiwa kutinga fainali ya mashindano ya Mapinduzi yanayoendelea Visiwani Zanzibar baada ha kuiondoa Singida Fountains Gate kwa penati 3 - 2.

FT: Singida Fontaine Gate FC 1-1 Simba SC

⚽️Elvis Rupia 11'

⚽️Fabrice Ngoma 90+7'

Simba SC itachuana na Mlandege FC kwenye mchezo wa Fainali.

Penati za Simba:

Luis Miquissone ✅

Israel Mwenda ✅

Shomari Kapombe ❌

Moses Phiri ✅

Sadio Kanoute ❌

Penati za Singida FG:

Gadiel Michael ❌

Abdulmajid Mangalo ❌

Duke Abuya ✅

Deus Kaseke ✅

Medie Kagere ❌

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo, kipa wa Simba, Ally Salim Katoro amefunguka siri ya kudaka penati tatu za Kagere, Mangaro na Gadiel Michael.

“Mchezo ulikuwa mgumu kama mlivyoona, Singida walikuja kwa nguvu zote lakini tunshukuru tumeibuka na ushindi baada ya dakika 90 na kuingia fainali.

“Hakuna siri nyingine zaidi ya kujituma kwenye mazoezi na kusikiliza maelekezo ya mwalimu. Mwalimu wetu Cadena huwa tunamshukuru sana, anafanya kazi kubwa sana.

“Nilijua Medie Kagere, Gadiel Michael wananifahamu na mimi ninawafahamu namna wanavyopiga, mwalimu alinielekeza cha kufanya. Mechi zote huwa ananielekeza ikitokea penati unatakiwa ufanye hivi na hivi, amenielekeza nikafanya na tukafanikiwa.

“Sio Singida tu, timu yoyote ikitokea tukaenda kwenye penati, cha kwanza ni kutokuwa na wasiwasi hata kidogo. Mwenye asilimia kubwa ni mchezaji lakini kipa ana asilimia chache sana kama 25 tu. Mimi huwa sina wasiwasi hata nikifungwa.

“Baada ya mchezo nimepewa pesa nyingi lakini zote nimegawa nimebakiwa na Tsh 32,000 tu, mtu mwingine asiniombe pesa,” amesema Ally Salim.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live