Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ally Kamwe awatolea povu waandishi wa habari

Ally Kamweoct 7 Ally Kamwe awatolea povu waandishi wa habari

Thu, 1 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Afisa Habari wa Yanga SC, Ally Kamwe amewatolea uvivu waandishi wa habari kwa kusema, wameshindwa kuripoti vizuri rekodi yao ya unbeaten na badala yake, wameungana kuishangilia Ihefu iliyopata ushindi dhidi ya mabigwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kamwe ametoa kauli hiyo leo Desemba Mosi, 2022 alipokuwa akifanya mahojiano na Wasafi FM akinadi mchezo wao dhidi ya Tanzania Prisons unaotarajiwa kufanyika Jumapili hii katika Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar.

"Unajua hamkututendea haki Yanga Africans, mlipaswa kutenga muda hata wa lisaa kujadili rekodi yetu ambayo tumeiweka, mlipaswa kuchambua kwa umakini ni rekodi ambayo sidhani kama inaweza kuwekwa tena nchini labda turudie sisi wenyewe," alisema Ally.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live