Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ally Kamwe awaita mashabiki Tanga

Image 61 1140x640.png Mashabiki wa Yanga

Mon, 7 Aug 2023 Chanzo: Dar24

Uongozi wa Young Africans umetamba kuwa kama watu walidhani walifanikiwa kuiona Young Africans ya Gamondi basi wamejidanganya, kwani Young Africans ya Gamondi itaonekana kule Tanga.

Kikosi cha Young Africans leo Jumatatu (Agosti 07) kinatarajia kusafiri kuelekea mkoani Tanga tayari kwa michezo yao ya Ngao ya Jamii wataanza kwa kucheza na Azam FC keshokutwa Jumatano (Agosti 09) Uwanja wa CCM Mkwakwani.

Young Africans itaingia kwenye mchezo huo wa Nusu Fainali ikiwa na kumbukumbu ya kutwaa ubingwa wa Ngao ya Jamii msimu uliopita baada ya kuifunga Simba SC mabao 2-1 mabao yote yakifungwa na Fiston Mayele.

Wakati huo Young Africans ilikuwa chini ya kocha Nasredinne Nabi sasa ni Miguel Gamondi raia wa Argentina.

Afisa Habari wa Young Africans, Ally Kamwe amesema kuwa: “Kama watu wanahisi waliiona Young Africans ya Gamondi basi wafahamu kuwa walijidanganya na niwaambie kuwa Young Africans ya Gamondi itapatikana kule Tanga.

“Young Africans ya Gamondi mtaiona Tanga ambayo inacheza mpira mzuri na wakuvutia, watu wengi waliiona Young Africans ya Gamondi ikicheza na Kaizer Chiefs ile sio Young Africans ya Gamondi.

“Watu wanaichukulia poa Young Africans lakini lazima wakubali mziki wa Young Africans kule Tanga na baada ya hapo wataanza kuipa heshima yake ambayo tuliipata msimu uliopita.”

Chanzo: Dar24
Related Articles: