Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ally Kamwe amtaka Kocha APR kuomba radhi

Alikamweeee Ally Kamwe amtaka Kocha APR kuomba radhi

Thu, 11 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga SC, Ally Kamwe amemtaka Kocha Msaidizi wa Klabu ya APR ya Rwanda, Aime Ndizeye raia wa Ufaransa kuomba radhi kutokana na kauli yake ya kuyaponda mashindano ya Mapinduzi Cup baada ya kutolewa na Mlandege FC kwa mikwaju ya penati juzi.

Akizungumza na wanahabari baada ya mchezo huo kumalizika, Ndizeye alisema kuwa waamuzi wameipendelea Mlandege na kuwanyima bao la wazi APR hivyo akasema iwapo waandaaji wa michuano hiyo hawatalifanyia kazi suala hilo basi APR hawatashiriki tena michuano hiyo.

Kwa upande wake, Ally Kamwe ambaye anaiwakilisha Yanga waliotolewa na APR kwenye hatua ya robo fainali ya michuano hiyo kwa kufungwa bao 3-1 amemtaka kocha huyo kuomba radhi kwani ameishushia hadhi michuano hiyo yenye heshima kubwa Afrika Mashariki na kati.

"Mapinduzi Cup ni mashindano maalum yenye heshima kubwa hapa Afrika Mashariki na Kati, timu nyingi kubwa, wachezaji wengi wakubwa wameshiriki. Tunapaswa kuyalinda, kuyaheshimu kwa nguvu zetu zote.

"Hata mtu anapotaka kuyaongelea ni lazima ayaongelee kwa nidhamu, isionekane mtu anakuja kushiriki kama 'msaada' tu kwa wenye mashindano. Hii sio sawa kabisa.

"Mistake za waamuzi kwenye Football zinatokea mpaka World Cup. Hata ujio wa VAR bado kuna makosa mengi ya waamuzi yametokea. Inakuaje mtu mwenye Taaluma ya ukocha anayakosea heshima mashindano ya Mapinduzi kirahisi tu kwa sababu ya waamuzi?

"Video hapo juu (Ipo kwenye ukurasa wa Ally Kamwe Instagram) Timu yake ya APR ilipewa BAO LA MCHONGO dhidi ya JKU kutoka ZANZIBAR mbona hakusema hatushiriki tena kwa sababu waamuzi wanatupendelea?

"Wakikosea waamuzi kwa wengine meno yote nje na kujiona bonge la Kocha. Wanashangilia mpaka wanavua nguo uwanjani. Wakikosea wengine Mnasusa?

"Sasa kwa tukio la jana (juzi) na hilo hapo la mechi ya JKU lipi lina upendeleo wa wazi kabisa? Nafikiri Kocha wa APR anatakiwa KUOMBA MSAHAMA HADHARANI kwa kauli yake.

"MAPINDUZI CUP ni Tournament ambayo kila mmoja wetu anapoyaongelea anatakiwa kuyaongelea kwa heshima. PERIOD. Mwenyekiti wa Wasemaji Afrika, Ally Kamwe," ameandika Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live