Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ally Kamwe amlipua vibaya Ahmed Ally kuwaponda wachezaji

Ally Kamwe 10 Goals Ally Kamwe amlipua vibaya Ahmed Ally kuwaponda wachezaji

Sun, 24 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ally kamwe ameijia juu Interview ya Ahmedy Ally aliyoifanya jana baada ya Simba kupata Sare dhidi ya Kmc akisema wachezaji wao hawajitumi. Kupitia Instagram Ally kamwe aliandika ujumbe huu kwa Ahmed Ally

"Shida ni kwamba .. Timu inaposhinda Msemaji unajimilikisha ushindi huo. Unatamba nao na kujipa kila aina ya majina kuonyesha kwamba Wewe ni KILA KITU kwenye Ushindi.

Lakini timu inapopata matokeo mabaya, Unajitenga nayo. Unaanza kutupa lawama hadharani kwa wachezaji kuwa hawana Ubora na Uchu wa kuipa Timu mafanikio..Huku ni KUKOSA HESHIMA.

Ni Ubinafsi na unaonyesha ni kwa kiasi gani Msemaji upo kwa ajili ya kulijenga jina lako na sio kuijenga Taasisi yako. Na hii ni mbaya pindi Interest binafsi zinapotangulia kuliko Interest za Taasisi.

Jambo moja ambalo inatupasa tuelewe, Nyakati nzuri na mbaya ni kwa ajili ya wote. Hakuna mchezaji anayekwenda uwanjani ili apoteze mchezo.

Kuwazodoa na kuwasema hadharani wachezaji wako ni kutaka kuwachonganisha na mashabiki. Ni ishara pia ya kutoheshimu kazi yao.

Na hata inapobidi, wachezaji wakatakiwa kusemwa, mwenye jukumu hilo ni Mkuu wa Benchi la Ufundi, Sio msemaji wa Timu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live