Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe ametupa dongo wa watani wao Simba Sc akidai kuwa timu hiyo ipo kwenye dalili za kukata pumzi ya mwisho.
Kauli hiyo ya Kamwe inakuja baada ya msemaji wa Simba, Ahmed Ally kudai kuwa michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika wanayoshiriki Yanga, ni midogo ambapo Simba haitaki wala hana mpango nayo.
“Nimesikia maneno maneno yameanza, sijui Kombe dogo, sijui vipi, sisi ambao tumesoma sana Dini hiyo ni ishara ya mwanadamu anayeelekea Sakaratul Maut, yaani mwanadamu anaelekea kwenye siku zake za mwisho, pumzi yake ya mwisho.
“Tukawatazama tukasema hee mashindano haya si ndio mlichoma uwanja nyie, mashindano haya yaliwapa goli bora wakalala wiki nzima wanalizungumzia tukasema hii dalili ya Sakaratul Maut.
“Kila mtu amalize shughuli aliyoianza walianza shughuli yao na Mwarabu wamalizane nao, tumeanza na Mnigeria tutamalizana nao tusizungumziane.
“Kombe dogo sijui kubwa ni la kwetu, kila mtu acheze Kombe lake, hili Kombe la Shirikisho ni la kwetu na tutalibeba,” Afisa Habari na Mawasiliano wa Yanga Sc, Ally Kamwe.