Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ally Kamwe: Tutamaliza kazi tuliyoianza Nigeria

Ally Kamwe Kijembe Ally Kamwe

Thu, 27 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amewataka mashabiki kununua tiketi kwa wingi ili kuhakikisha wanaujaza uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya Jumapili, April 30 katika mchezo wa mkondo wa pili robo fainali kombe la Shirikisho dhidi ya Rivers United

Baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Rivers United ugenini huko Nigeria, Kamwe amesema wanahitaji kumaliza kazi waliyoianza na kujihakikishia tiketi ya kucheza nusu fainali

Aidha Kamwe amewapiga 'dongo' wanaobeza michuano ya Shirikisho kuwa nao wanapaswa kwenda kuzima moto waliouwasha dhidi ya Waarabu, kuongelea mashindano ya wengine ni dalili ya kushindwa

"Nimesikia maneno maneno yameanza, sijui Kombe dogo, sijui vipi, sisi ambao tumesoma sana dini hiyo ni ishara ya mwanadamu anayeelekea Sakaratul Maut, yaani mwanadamu anaelekea kwenye siku zake za mwisho, Pumzi yake ya mwisho"

"Tukawatazama tukasema, mashindano haya si ndio mlichoma uwanja nyie, mashindano haya yaliwapa goli bora wakalala wiki nzima wanalizungumzia!"

"Kila mtu amalize shughuli aliyoianza walianza shughuli yao na Mwarabu wamalizane nao, tumeanza na Mnigeria tutamalizana nao tusizungumziane"

"Kombe dogo sijui kubwa ni la kwetu, kila mtu acheze Kombe lake, hili Kombe la Shirikisho ni la kwetu na tutalibeba," alitamba Kamwe

Chanzo: www.tanzaniaweb.live