Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ally Kamwe: Sitasahau hili msimu 2022/23

Ally Kamwe X Fei Toto Kumb Ally Kamwe: Sitasahau hili msimu 2022/23

Tue, 13 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe leo amefunguka matukio mawili ambayo hatoyasahau msimu uliomalizika wa 2022/23 akitaja moja ni sakata la mchezaji Feisal Salum ambaye alikuwa na mgogoro na timu hiyo kuvunja mkataba wake ili aende klabu nyingine ambapo sasa ni mchezaji wa Azam.

Meneja Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe leo amefunguka matukio mawili ambayo hatoyasahau msimu uliomalizika wa 2022/23 akitaja moja ni sakata la mchezaji Feisal Salum ambaye alikuwa na mgogoro na timu hiyo kuvunja mkataba wake ili aende klabu nyingine ambapo sasa ni mchezaji wa Azam. Kamwe akihojiwa na Azam Tv amesema la pili ni walipopata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar uwanja wa CCM Kirumba likifungwa na Clement Mzize Novemba 13 mwaka jana wakitokea Tunisia kucheza dhidi ya Club Africain Novemba 9 walipotinga hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuifunga bao 1-0.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: