Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ally Kamwe: Pacome aliwavuruga Azam FC

Dabo Pacome Ally Kamwe: Pacome aliwavuruga Azam FC

Wed, 25 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Klabu ya Azam, Youssoupha Dabo juzi alionekana akiwaita wachezaji wake nje ya uwanja na kuwapa maelekezo mara baada ya kusawadhisha bao lao dhidi ya Yanga SC katika Dimba la Mkapa.

Dabo alionekana akishika kichwa chake jambo ambalo limetafsiriwa kuwa huenda alikuwa akiwaelekeza kumkaba kiungo wa Yanga, Pacome Zouzoua raia wa Ivory Coast aliyeonekana kuwa mwiba kwa viungo wa Azam.

Akizungumzia tukio Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe amesema kuwa hali ilikuwa mbaya kwa Azam kiasi cha kushindwa hata kuelewana kwa lugha ya maneno hivyo kocha wao akaamua kutumia lugha ya ishara kuwaelekeza wachezaji wao namna ya kumkaba Pacome.

"Yanga ni klabu ya taifa inahudumia mpira wa Tanzania kwenye eneo la burudani, na tunajua wagonjwa ni wengi ila ukifika mechi za Yanga wauguzi kwenye mahospitali wanaweka mechi ili wagonjwa waangalie, kwa hiyo waje zaidi na zaidi.

“Baada ya Sillah kuisawadhishia Azam, kocha wao Dabo aliwaita wachezaji wake akina Akaminko na Bajana akawaambia sasa hivi tumesawadhisha, Yanga wata-react, sasa waki-react nani ni mtu hatari?

“Wale ni viungo wakabaji na Pacome ni kiungo mshambuliaji kwa hiyo Dabo apozungumza kwa maneno akaona kama hawamuelewi, ndipo akasema ‘jamani yule mwenye ma-brichi’ walipomfata Pacome akawa kama Jet Lee.

“Pacome aliwachanganya sana Azam FC mpaka kocha wa Azam akwaita wachezaji wake kuwapa maelekezo ilikuwa hatari Uwanjani,” amesema Ally Kamwe.

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya NBC, Yanga iliibuka na ushindi wa bao 3-2 dhidi ya Azam, mabao yote ya Yanga yakifungwa na Aziz Ki wakati mabao ya Azam yakifungwa na Gibril Sillah na Prince Dube kwa mkwaju wa penati.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: