Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ally Kamwe: Kuiogopa Al Hilal ni kichekesho

Kamwe Ally.png Ally Kamwe

Thu, 29 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Afisa Habari mpya wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe amesema kuwa wapinzani wao kwenye mchezo wa unaofuata wa Ligi ya Mabingwa, Al Hilal ni timu ndogo sana tofauti na inavyozungumziwa na wachambuzi wa soka.

Ally Kamwe ameyasema hayo wakati akihojiwa kuhusu mechi hiyo na kuongeza kuwa Yanga kwa sasa ina wachezaji bora kuliko Al Hilal na tayari wana muunganiko mzuri na becnhi la ufundi imara, hivyo kupenya katika makundi kwa yanga msimu huu ni jambo la lazima.

Yanga itashuka kwenye Uwanja wa Mkapa, Oktoba 8, 2022 kukabiliana na Al Hilal kutoka Sudan ambayo inafundishwa na aliyekuwa kocha wa AS Vita kisha RS Berkane, Florent Ibenge raia wa Congo DR.

"Malengo makubwa ya Yanga ni kucheza Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Kama una malengo hayo halafu unaihofia Al Hilal, utakuwa unachekesha.

"Siamini kama timu ya Al Hilal inapaswa kuipasua kichwa Yanga, tayari Yanga ni Ttimu kubwa sana. Hatua ambayo wanapitia Al Hilal kwa sasa kutengeneza timu Yanga ilishapitia miaka minne (4) nyuma.

"Sisi tayari tunawachezaji wazuri na tuna timu nzuri, wenzetu wana wachezaji wazuri, wanajitafuta kutengeneza timu nzuri. Yanga sio timu ya kuumiza kichwa kuifikiria Al Hilal,” amesema Ally Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live