Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ally Kamwe: Huu ni msimu mgumu kwa Yanga

Kamwe Msh Ally Kamwe: Huu ni msimu mgumu kwa Yanga

Wed, 13 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msemaji wa Klabu ya Yanga, Ally Shabani Kamwe amesema msimu huu ni mgumu kwa timu yao kutokana na kuongezeka kwa michuano mikubwa ya Kimataifa (Ligi ya Mabingwa Afrika) ambayo hawakuwa wakishiriki misimu 25 iliyopita.

Kamwe amesema licha ya hayo, bado mahasidi wameongezeka ambao wamekuwa wakiitakia mabaya timu hiyo ambayo ni mabingwa wa muda wote wa Ligi Kuu ya Tanzania na mabingwa watetezi.

“Kama kuna msimu mgumu, basi ni huu wa 2023/2024, kwa sababu tupo kwenye michuano mikubwa Afrika, lakini pia kwenye ligi ya ndani hasadi zimekuwa nyingi kwelikweli, roho mbaya zimeongezeka.

“Sifa ya kwanza ya mtu mwenye roho mbaya hana uwezo, kwa hiyo kama hana uwezo anaomba mfanane, kwa mfano sisi Yanga michuano ya CAF tunaumizwa kuwa na pointi mbili, lakini kwa sababu wenzetu hawana uwezo sifa yao ni roho mbaya, wanafurahia wote tuko chini.

“Wao wanasikia raha, wanasema mlisema mna timu nzuri mbona mko chini kama sisi, wao wanasikia raha, maana yake tuna vita kubwa ya kupigana kama Wanayanga.

“Vita yetu ni kubwa mno, kama hatutakuwa pamoja kushikana, kupigana vita hiyo tutabaki chini wote kama wenzetu, wao watakuwa wamefanikiwa kuiweka Yanga chini, sasa tisikubali hilo jambo,” amesema Ally Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live