Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ally Kamwe: Azam wamekosa weledi

Mzize SEEofz Ally Kamwe: Azam wamekosa weledi

Mon, 22 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe amesema kuwa Klabu ya Azam imekosa weledi kwa kuanza kumtangaza mshambuliaji wa Yanga Clement Mzize kuwa ni wao.

Kauli hiyo ya Kamwe inakuja baada ya msemaji wa Azam FC, Hasheem Ibwe kudai kuwa wameshatuma ofa nono kwa Yanga kutaka kumsajili Mzize.

"Mzize bado ana mkataba na Yanga tena ambao hamruhusu kuongea na timu nyingine ila ofa zinazokuja klabuni za kutaka kumnunua, lakini kauli ambazo zinatolewa na viongozi wa Azam FC kuwa wametuma ofa nono tena hadharani kisha wanasema wanaenda uwanjani kumuangalia mchezaji wao wakati hata ofa yao haijakubaliwa, lakini wanamuita Mzize no mchezaji wetu, haya mambo hayafanyiki popote Duniani.

"Sijawahi kuona timu yoyote Ulaya mfano Real Madrid wanatoa taarifa katikati ya msimu kuwa wametuma ofa kwa mchezaji wa timu nyingine hii ndo naona kwa mara ya kwanza kwetu Tanzania, tena viongozi wa timu (msemaji) wao anamuita Mzize ni mchezaji wetu.

"Yaani Madrid isafiri iende England ikamuangalie mchezaji ambae ofa yake haijakubaliwa na wakati huohuo tayari wanamuita mchezaji wao, hii sijawahi kuona, sasa isije baadae tukafanya sisi mkasema hatuna Weledi," amesema Ali Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live