Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ally Kamwe: Aucho amerejea, yuko fiti

Aucho Df Khalid Aucho

Tue, 24 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga imesema kiungo wake raia wa Uganda, Khalid Aucho amepona majeraha yake na tayari ameshaanza mazoezi ya gym kwa programu maalum ya mwalimu kabla ya kujiunga na wenzake mazoezini.

Hayo yamesemwa leo Jumanne, Januari 24, 2023 na Ofisa Habari wa Klabu hiyo, Ally Kamwe wakati akizungumza na Yanga TV kuhusu hali ya AUcho ambaye aliumia mazoezini wiki iliyopita kabla ya mchezo wao na Ihefu FC.

"Khalid Aucho ameshapona majeraha yake na ameanza mazoezi ya kurejesha utimamu wake wa mwili kuanzia wiki iliyopita. Alikuwa na program tofauti tofauti na leo alikuwa na mtaalam wetu wa voiungo pale Gymkana.

"Lengo ni kujiweka fiti kabla hajaungana na wenzake kikosini kwa ajili ya mazoezi ya jumla ya kikosi kizima. Auchop yupo fiti, soon atarejea dimbani" amesma Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live