Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alliance Girls, Tigers Queens ngoma ngumu

Alliance Pic Data Alliance Girls imekutana na kigingi ikilazimishwa suluhu na The Tigers

Mon, 27 Dec 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Baada ya kuanza kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mlandizi Queens, leo Alliance Girls imekutana na kigingi ikilazimishwa suluhu na The Tigers ya jijini Arusha.

Mchezo huo wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara umepigwa leo kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza huku wageni wakikosa nafasi za wazi za kufunga mabao.

The Tigers ambao walishinda mchezo wao wa kwanza kwa mabao 4-0 mbele ya TSC ya Mwanza, walitengeneza nafasi nyingi za mabao ambapo mshambuliaji wao Amina Ramadhan alikosa nafasi mbili za wazi moja akiwa yeye na kipa na nyingine akiwa peke yake na nyavu lakini akapiga nje.

Alliance nao walijaribu kujitutumua kutengeneza nafasi lakini walishindwa kifua dafu mbele ya mabeki wa Tigers waliocheza kwa kuelewana vyema na kuondoa hatari zote.

Hadi dakika 90 za mtanange huo zinamalizika timu hizo zimegawana alama moja huku Onesta Hamidu wa Tigers akilimwa kadi nyekundu kwa kufunga bao kwa mkono, ambapo timu hizo zinafikisha pointi nne nyuma ya vinara Simba Queens iliyoshinda mechi zake mbili.

Kocha wa Alliance Girls, Sultan Juma amesema ameridhishwa na kiwango cha wachezaji wake katika mechi hizo mbili huku akijipanga zaidi kwa mchezo ujao wa ugenini dhidi ya Ruvuma Queens, huku Kocha wa Tigers Alex Alumirah akilaumu washambuliaji wake kwa kupoteza umakini katika eneo la mwisho.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz