Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Allardyce atoa povu Man United kisa Haaland

Sam Pic Data Sam Allardyce

Mon, 31 Jan 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Mkongwe wa soka Sam Allardyce, amewaponda mabosi wa Manchester United kwa uzembe wao wa kukosa kunasa saini ya nyota anayekipiga Borussia Dortmund, Erling Haaland mwaka 2020.

Man United ilikuwa na nafasi nzuri ya kunasa saini ya mkali huyo wa mabao Bundesliga kwenye dirisha dogo Januari mwaka juzi, lakini ikagonga mwamba, Borussia Dortmund ikiwapiku na kumng’oa, kipindi hicho akikipiga RB Sulzburg msimu wa 2019-2020.

Kwa mujibu wa ripoti, Man United ilikuwa mbioni kumsajili Haaland, tangu mwaka 2018, lakini kutokana na sababu mbalimbali zilizojitokea ilichangia dili hilo kubuma kabla ya RB Sulzburg kuingilia kati na kufanikiwa kumsajili.

Haaland tangu alipotua Bundesliga amekuwa moto wa kuotea mbali na ameshaweka kambani mabao 16 katika michezo 14 aliyocheza msimu huu.

Lakini, Allardyce amesikitishwa kwanini Man United imeshindwa kumsajili Haaland huku akiamini endapo Mashetani Wekundu wangefanikia basi Ole Gunnar Solskjaer kibarua chake kisingeota nyasi Old Trafford.

“Nilidhani Man United wangemchukua Haaland, Solskjaer alikuwa na nafasi nzuri kwa sababu anamfahamu tangu anaanza soka, nimeshangaa kwanini walishindwa kutoa pesa, wamefanya makosa makubwa sana kumkosa mchezaji huyo, nadhani Solskajer asingefukuzwa kama angempata,” alisema Allardyce.

Man United imemkosa Haaland kama masihara, ambaye tangu anatua Borussia Dortmund, amefunga mabao 80 katika mechi 70 alizocheza huku Allardyce akisisitiza Real Madrid na Manchester City wanaweza kuchuana vikali kuiwania saini yake mwisho wa msimu huu.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz