Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyoyafanya kwa Fei Toto kwa Yanga ndiyo anayafanya Dube kwa Azam

Prince Dube Ms Aliyoyafanya kwa Fei Toto kwa Yanga ndiyo anayafanya Dube kwa Azam

Tue, 5 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kama unakumbukumbu vizuri niliwahi kuandika hapa wakati ule wa sakata la Feisal Salum kushinikiza kuvunja mkataba na Yanga kwenda Azam FC kinyume na utaratibu.

Nilisema, hili wanalolifanya Azam FC na Yusuf Bakhresa wanatengeneza kansa Mbaya kwenye Soka la Tanzania, haitaishia kwa Yanga tu kama baadhi ya watu wanavyoamini, kansa itaendelea kutafuna katika vilabu mbalimbali.

Baadhi ya watu wenye mihemko na unazi walinicheka wakiamini labda nimechanganyikiwa.

Mungu si mzee Mkumba hata mwaka na nusu haujaisha ile kansa niliyoisema imeanza kutafuna, tena imeanza na Azam FC wao wenyewe.

Sakata la Prince Dube kushinikiza kuvunja Mkata na Azam FC linafanana Exactly kama la Feisal. Azam wanahaha muda huu, wamesahau CARMA IS A BITCH.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live