Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyeuawa kwenye mechi Ubelgiji alikuwa mfungwa aliyetoroka gerezani

Abdesalem Lassoued.jpeg Abdesalem Lassoued.

Tue, 24 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taarifa kutokea Ubelgiji zinaeleza kuwa Abdesalem Lassoued, Mwanaume aliyeua raia wawili wa Sweden jijini Brussels wiki iliyopita, alikuwa ni mfungwa aliyetoroka Tunisia.

Jumatatu ya tarehe 16 Oktoba, mwanaume huyo aliwashambulia kwa risasi wapita njia katikati ya Mji Mkuu wa Ubelgiji, na kuwaua raia wawili wa Sweden na kumjeruhi mtu mwingine mmoja.

Marehemu walikuwa jijini humo kwa ajili ya mechi kati ya Ubelgiji na Sweden ya kuwania kuingia kwenye Michuano ya Euro 2024.

Baada ya msako mkali mhalifu huyo alikutwa Jumanne asubuhi katika Mgahawa karibu na nyumbani kwake, ambapo aliuawa kwa kupigwa risasi na polisi.

Mwendesha Mashtaka nchini Ubelgiji amesema kuwa mwaka 2015 Abdesalem alihukumiwa kifungo cha miaka 26 jela kwa uhalifu ikiwemo njama za kuua.

Alitoroka mwaka 2011, akafanikiwa kusafiri kwa boti ndogo na kuingia Ulaya kwa kupitia kisiwa cha Lampedusa kilichopo nchini Italia,kinyume na sheria.

Baadaye alihamia Ubelgiji ambapo aliomba kuwa mkimbizi na kukataliwa.

Mnamo Agosti mwaka jana, Mamlaka nchini Tunisia ziliiomba Ubelgiji kumrudisha mfungwa huyo, ombi ambalo lilipokelewa lakini halikushughulikiwa.

Wiki iliyopita Waziri wa Haki wa Ubelgiji Vincent Van Quickenborne alijiuzulu na kuwaomba radhi sana waathirika wa shambulio hili, huku akisema “kilichotokea ni makosa makubwa, yasiyokubalika na yenye madhara makubwa”.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live