Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyetoroka kambini na mpenzi wake afunguka

Atorkaaaaaaaaaaaaaaaaaa Aliyetoroka kambini na mpenzi wake afunguka

Thu, 1 Aug 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mwogeleaji wa Brazil ambaye alifukuzwa kwenye Michezo ya Olimpiki baada ya kutoroka kambini akiwa na mpenzi wake 'kwenda kula bata katika mitaa ya Paris, usiku' amevunja ukimya.

Ana Carolina Vieira na Gabriel Santos walidaiwa kuondoka kambini Julai 26, bila kibali hali iliyosababisha waitwe katika kamati ya nidhamu ya baraza la michezo ya majini na walipewa adhabu ya kuondolewa katika michezo ya Olimpiki na kurudishwa nyumbani.

Hata hivyo, baada ya adhabu hiyo, Carolina alipinga papo hapo na kuiambia kamati hawastahili kuadhibiwa hivyo.

Katika taarifa iliyotolewa na baraza la Michezo ya Majini nchini Brazil, (CBDA), ilisema kamati ya nidhamu iliwaadhibu waogeleaji hao wawili kwa kuwarudisha nyumbani.

"Licha ya kuadhibiwa, mchezaji Ana Carolina, kwa njia ya dharau na fujo, alipinga uamuzi wa kamati, baada ya tukio hilo, kamati ikampa onyo Gabriel Santos kisha ikamuadhibu Carolina kwa kumfukuza kambini na kumtaka arejee Brazil mara moja."

Carolina amefunguka kuhusu suala hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram na kusema alifanyiwa unyanyasaji wa kijinsi na ataenda kufungua mashtaka dhidi ya kamati na baraza kijumla.

"Niliondoka pale na kuacha vifaa vyangu, sikujua la kufanya. Vitu vyangu viko huko kambini, nilienda kwenye uwanja wa ndege nikiwa na nguo fupi. Ilibidi nifungue koti langu na kujifunga kwa sasa niko Ureno ila nitarudi Brazil. Sina msaada, sijapata chochote, sijaweza kuongea na mtu yeyote. Nitazungumza na wanasheria wangu. Ninaahidi kusema kila kitu."

Akizungumzia ukiukaji wa sheria hiyo, kiongozi wa timu ya kuogelea ya Brazil, Gustavo Otsuka aliiambia Reuters: "Hatupo hapa kucheza au kuchukua likizo. Tupo hapa kufanya kazi kwa ajili ya walipa kodi milioni 200 wanaotufanyia kazi. Hatuwezi kucheza hapa."

Chanzo: Mwanaspoti