Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyetakiwa kuibiwa Airport ni Pacome sio Ngoma

Pacome Ngoma Aliyetakiwa kuibiwa Airport ni Pacome sio Ngoma

Thu, 9 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shabiki kindakindaki wa Klabu ya yanga, Muniain Samangwana maarufu kama Gody Yanga amesema kuwa mchezaji aliyetakiwa kuibiwa Uwanja wa Ndege ni kiungo wa Yanga Raia wa Ivory Coast, Pacome Zouzouana siyo Fabrice Ngoma wa Simba.

Gody amesema hayo kufuatia kiwango bora ambacho amekionyesha Pacome tangu atue Yanga msimu huu hasa kwenye mchezo wa Dabi ya Kariakoo ambapo Yanga iliifunga Simba bao 5-1.

Awali wakati wa dirisha la usajili, viongozi wa Simba walijinasibu kuwa walimuiba Ngoma ambaye ni raia wa Congo DR katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kumsainisha mkataba, hivyo akaiacha Yanga kwenye mataa.

"Simba wamefungwa mabao ya kimpira, wamezidiwa ubora na Yanga pakubwa sana. Hili tulikuwa tunawaambia wakati wa usajili kwamba wajitahidi kuangalia ubora wa wachezaji na si kufurahisha midomo ya watu.

"Kipindi cha usajili msemaji wao anakuja anawadanganya kuhusu Che Fondoh Malone, anawadanganya kuhusu Fabrice Ngoma kaibiwa Airport, lakini huo ubora hauonekanai uwanjani.

"Usajili mzima ni wachezaji wawili tu walioingia kwenye kikosi cha kwanza, Ngoma na Malone na bado hawana viwango vikubwa kama wachezaji wa Yanga au Azam.

"Muangalie Ngoma na Pacome halafu uniambie nani kwenye quality kubwa na alistahili kuibiwa Airport? Unagundua Pacome Zouzoua ndiye mchezaji aliyetakiwa kuibiwa na upande wowote ambao ungekuwa na pesa ya kumshawishi," amesema God Yanga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live