Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyeshiriki 5-0 za Simba aamsha morali Tabora United

Mbomboooooo Nelson Omba Munganga

Wed, 24 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha Mkuu wa Tabora United, Goran Kopunovic amesema amefurahishwa na usajili uliofanywa wa kiungo Mkongomani, Nelson Omba Munganga aliyetokea klabu ya DC Motema Pembe katika dirisha dogo la usajili lililofungwa Januari 16, mwaka huu.

Akizungumza na Mwanaspoti, Goran alisema usajili wa nyota huyo ni miongoni mwa mapendekezo yake hivyo amepongeza uongozi kwa kufanikisha kumpata kwani atasaidia kuongeza nguvu katika kikosi hicho kinachoendelea na mazoezi mkoani Shinyanga.

“Kila mmoja wetu anatambua ubora wake na natambua haikuwa rahisi kupata saini yake kwa sababu ninafahamu baadhi ya klabu nyingine zilikuwa zinamuhitaji, hivyo nitoe pongezi kwa viongozi kwa kupata mchezaji mkubwa na mzoefu kwetu,” alisema.

Kuhusu maandalizi yanayoendelea Shinyanga, Goran aliongeza hali ya kambi hiyo inaendelea vizuri na wachezaji wote kwa pamoja wako kwenye morali kubwa huku akibainisha malengo yao ni kumaliza nafasi nne za juu katika Ligi Kuu Bara msimu huu.

“Tuna wiki kadhaa kabla ya kurudi katika michezo ya kiushindani ndio maana tumeanza maandalizi mapema ili kujiweka fiti kwa ajili ya kuleta ushindani, hadi sasa hatujafanya vizuri au vibaya sana hivyo tunayafanyia kasi mapungufu yetu yote.”

Nyota huyo kabla ya kuichezea DC Motema Pembe ila amewahi kuichezea AS Vita Club ya kwao nchini Congo na Maghreb de Fes ya Morocco huku akicheza michezo 34 ya Ligi ya Mabingwa Afrika, 14 ya Kombe la Shirikisho Afrika na 12 ya timu ya Taifa.

Chanzo: Mwanaspoti