Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyempiga polisi shoka, apigwa risasi Ujerumani

Hamburg Kisu Aliyempiga polisi shoka, apigwa risasi Ujerumani

Sun, 16 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mwanaume mmoja anayedaiwa kuwa ni shabiki na aliyemshambulia askari polisi kwa shoka, huko Ujerumani inapofanyikia fainali za Euro 2024, amepigwa risasi.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka The Mirror ni kwamba, baada ya shabiki huyo kupigwa risasi aliingizwa katika gari ya kubebea wagonjwa na kuwahishwa hospitalini kwa ajili ya matibabu.

Tukio hili lililotokea muda ya saa 6:30 mchana, lilifanyika katika Mtaa wa Reeperbahn jijini Hamburg ambapo askari walikuwa wakifanya doria kwa ajili ya kuimalisha ulinzi.

Mtaa wa Reeperbahn ni moja kati ya mitaa maarufu jijini Humburg na hivi karibuni umekuwa na ongezeko la watu, wengi wao wakiwa ni mashabiki wa Poland na Uholanzi ambao timu zao zitacheza hatua ya makundi jijini humo.

Mwanaume huyo ambaye hajajulikana kuwa ni shabiki wa timu gani, alimpiga askari kwa shoka linalidaiwa kuwa na rangi ya dhahabu na baada ya kufanya hivyo, askari mwingine aliyekuwa karibu alijaribu kutumia dawa maalumu ya kupulizia wahalifu machoni ili kumtuliza, lakini hakufanikiwa.

Baada ya kuona mambo yanakuwa magumu kwa upande wao, askari huyo alitoa bunduki ndogo aliyokuwa nayo na kumpiga risasi mwanaume huyo.

Kutokana na tukio hilo, jeshi la Polisi jijini Hamburg ilitoa taarifa iliyoeleza: ”Kwa sasa kuna operesheni inayoendelea, kwa mujibu wa taarifa ni kwamba mwanaume huyo alikuwa akitishia kuwadhuru askari kwa shoka na silaha nyingine, hivyo ili kumtuliza ndio wakatumia bunduki walizokuwa nazo na mtu huyo alijeruhiwa na sasa anapatiwa matibabu hospitalini”

Mbali ya mechi za Poland na Uholanzi, mji huu pia ndio umetumika kwa ajili ya mechi ya ufunguzi ya England na Serbia.

Inaelezwa Uholanzi na Poland zimekuwa na kundi kubwa la mashabiki jijini Humburg kwa sababu mji huo upo mpakani mwa nchi hizo.

Kutokana na kuwa mpakani, imefanya watu husafiri kwa treni ndani ya muda mfupi tu na kuchangia ongezeko la watu.

Chanzo: Mwanaspoti