Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyempeleka Gadiel Michael Sauzi atimuliwa

Ernst Middendorp Sz Ernst Middendorp.

Wed, 5 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Cape Town Spurs imetangaza kuachana na Kocha wao Mkuu Ernst Middendorp baada ya kushindwa kuibakisha timu hiyo Ligi Kuu ya nchini Afrika Kusini.

Hivyo basi Cape Town Spurs imeshuka daraja na msimu ujao itacheza ligi daraja la kwanza maarufu kwa jina la Motsepe Foundation Championship.

Ikumbukwe Kocha huyo ndie aliyependekeza usajili wa nyota wa kimataifa wa Tanzania, Gadiel Michael klabuni hapo akitokea Singida Fountain Gate.

Je, tutarajie kurejea kwa beki huyo nyumbani au Kiwango chake ndio kitaamua Mustakhabali wake ndani ya Cape Town Spurs?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live