Aliyekuwa Mwenyekiti wa Yanga, wakili, Imani Madega anatarajiwa kuzikwa kesho saa 10:00 jioni nyumbani kwake Chalinze.
Mtoto wake Abdul Madega amezungumza kwamba baba yake alijisikia vibaya asubuhi na akamwambia ampeleke Hospital ya Wilaya ya Chalinze, Musoga.
"Leo asubuhi mzee alinipigia simu kuniambia anajisikia vibaya nimpeleke hospitali, nikafika kwa uharaka nyumbani, lakini alikuwa anatembea na nguvu zake kabisa, tukafika hospital akaanza kutibiwa maradhi ya presha,"
"Akawa anaendelea vizuri tu, baada ya kufika saa tano asubuhi, akaaga dunia, ndio maana nashindwa kueleza sana,"
"Watu wengi wanashangaa, maana juzi alienda Dar es Salaam, alipita kwa marafiki zake akiwa mzima, ingawa shida ya presha ilikuwa inamsumbua na alikuwa anahudhuria kliniki na kutokana na ukubwa wake ndio maana tumeamua azikwe kesho, ili watakaopata muda wahudhurie."