Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyeimba Tabulele... Laah kutua Bongo kuongoza hamasa Yanga

Kkl Bomoko Aliyeimba Tabulele... Laah kutua Bongo kuongoza hamasa Yanga

Mon, 27 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki wa Kundi la KKL Bomoko la nchini Congo aliyeimba kibao cha Tabulele... Laah atakuja nchini kwa ajili ya kuongoza hamasa ya mashabiki katika pambano la Yanga SC na Al Ahly.

Msanii huyo anakuja nchini Jumatano kuongoza hamasa hiyo kuelekea mchezo wao wa pili wa Klabu Bingwa Afrika utakaochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar Salaam.

Msanii huyo tayari amesharekodi remix ya wimbo huo na mmoja wa wasanii wakubwa hapa nchini na wimbo huo unatarajiwa kuachiwa Jumatano.

Je unadhani ni msanii gani ambaye atakuwa amehusishwa kwenye ngoma hiyo?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live