Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alisson Becker awakatalia Waarabu mchongo Saudia

Alisson Becker Alisson Becker awakatalia Waarabu mchongo Saudia

Thu, 13 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kipa wa Liverpool na Brazil Alisson Becker, 31, amekataa ofa ya kujiunga na Al Nassr ya Saudi Arabia katika dirisha hili baada ya kukutana na kocha mpya Arne Slot ambaye amemuomba aendelee kuwepo zo yake.

Becker ambaye bado ana mkataba wa kuitumikia Liverpool hadi mwaka 2027, hivi karibuni alihusishwa kuondoka baada ya Jurgen Klopp kutangaza kuachana na timu hiyo.

Al Nassr inaripotiwa kuwa ilikuwa tayari kumpa mshahara mara tatu zaidi ya ule ambao anaupokea kwa sasa akiwa na majogoo hao wa Jiji la Liverpool.

Awali, ilielezwa Becker anataka kuondoka na kwenda kupata changamoto mpya Saudia ambako ameahidiwa pesa nyingi.

Al Nassr inapambana kutafuta kipa na ilipanga ikiwa itashindikana kumpata nyanda huyu wa Liverpool basi itahamia kwa kipa wa Juventus.

Katika msimu uliomalizika, Becker alicheza mechi 32 za michuano yote na kuruhusu mabao 32 kutinga katika nyavu zake.

Chanzo: Mwanaspoti