Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliou Cisse freshi baada la kulazwa

Aliou Cisse 1140x640 Aliou Cisse.

Mon, 22 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa timu ya taifa ya Senegal, Aliou Cisse alipata matatizo ya kiafya, akawahishwa hospitalini kufuatia ushindi dhidi Cameroon, lakini sasa anaendelea vyema baada ya matibabu Ijumaa.

Simba wa Teranga waliendeleza mwanzo mzuri wa kutetea taji lao la Mataifa ya Afrika kwa ushindi wa mabao 3-1 na kutinga kibabe hatua ya 16-Bora.

Hata hivyo, Cisse alipata tatizo la kiafya na akapatiwa matibabu katika hospitali ya mjini Yamoussoukro ambako alilazwa usiku mzima.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 47 baada ya hapo aliruhusiwa kutoka hospitalini na kurejea kikosini kwake. Taarifa ya shirikisho la soka la Senegal ilisema: “Vipimo alivyofanyiwa vimemhakikishia yuko sawa na amerejea kundini.

“Anaendelea vyema,” msemaji wa timu ya Senegal, Kara Thioune aliongeza. Cisse amekuwa kocha wa timu ya taifa hilo tangu 2015 na aliiongoza kutwaa ubingwa wa AFCON katika fainali za 2022.

Alioongoza pia katika fainali mbili zilizopita za Kombe la Dunia, zikiwamo za mwaka juzi kule Qatar ambako walitolewa na England katika hatua ya 16-Bora.

Ismaila Sarr, Habib Diallo na Sadio Mane walifunga mabao ya Ijumaa wakati Senegal ikiichakaza Cameroon, ambayo bao lake la kufutia machozi lilifungwa na Jean-Charles Castelletto.

Senegal itacheza mechi ya kukamilisha ratiba dhidi ya Guinea kesho Jumanne kabla ya kumsubiri mpinzani wa 16-Bora. 

Chanzo: www.tanzaniaweb.live