Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliou Cissé kocha mkuu wa Senegal hadi 2026

Aliou Cisse 1140x640 Aliou Cissé.

Mon, 11 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa timu ya Taifa ya kandanda ya Senegal, Aliou Cissé, ameteuliwa tena kuwa Kocha Mkuu hadi mwaka wa 2026, lilitangaza Shirikisho la soka la Senegal (FSF) katika video iliyochapishwa Ijumaa Machi 8.

Kamati ya utendaji imeonyesha imani tena kwa kocha Aliou Cissé na inamtaka aendelee na kazi yake, malengo ikiwa ni kufuzu kwa AFCON 2025 na Kombe la Dunia la 2026,” alisema Makamu wa Rais wa Shirikisho Seydou Sane.

Senegal kwa sasa iko katika nafasi ya 17 katika viwango vya FIFA, nafasi ya pili kwa ubora barani Afrika baada ya Morocco ya 12.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live