Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alikiba achangia sh milioni 20 Taifa Stars

Alikiba King Alikiba achangia sh milioni 20 Taifa Stars

Thu, 11 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii maarufu wa Bongo Fleva, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Lebo ya muziki ya King Music, Alikiba amechangia kiasi cha Tsh milioni 20 katika hafla ya Harambee ya kuchangia timu ya Taifa (Taifa Stars).

Hafla hiyo ilifanyika jana usiku Januari 10, 2024, katika Hoteli ya Johari, Rotana iliyopo Jijini Dar es Salaam ili kuisapoti Stars ambayo ipo nchini Ivory Coast kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya Fainali za AFCON 2023 zitakazoanza januari 13, 2024.

Aidha, katika hafla hiyo, Rais Samia alichangia kiasi cha Tsh milioni 500 ni kuwaasa Watanzania wote kujitolea kuisaidia timu yao ya Taifa pamoja na michezo mingine.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live