Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alietunguliwa na Aziz Ki apata mtetezi

Mtibwa To Simba SC Kikosi cha Mtibwa Sugar

Wed, 4 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Juzi Jumapili Mtibwa Sugar ikiwa nyumbani ilishindwa kumzuia Yanga asiwafunge huku wengi wakimlaumu kipa Razack Shekimweri kushindwa kudaka shuti la Stephan Aziz KI lakini ametetewa.

Azizi KI aliifungia Yanga bao pekee kwa mpira wa adhabu ambao kipa wa Mtibwa alishindwa kuudaka hivyo kujikuta wakiiachia Yanga pointi tatu wakiwa nyumbani Manungu.

Kocha Msaidizi wa Mtibwa Sugar, Awadh Juma alisema kipa wao alikuwa na uwezo wa kuudaka mpira lakini alishindwa kufanya hivyo kutokana na kutokuwa na uwezo mkubwa wa kudaka mipira ya aina hiyo.

“Kabla ya kufungwa bao tulikuwa tunaenda vizuri, tulimiliki mpira lakini kipa wetu alishindwa kudaka mpira aliopiga Azizi KI kutokana na uzoefu wake kuwa mdogo, ule mpira ulikuwa ndani ya uwezo wake lakini alishindwa kuudaka na Yanga wakamaliza mchezo.

“Dirisha la usajili linaendelea na tuna mpango wa kuboresha kikosi chetu na tumefanya scouting ya wachezaji hivyo tutaongeza kwa mapungufu tuliyonayo. Tukiwapata wale tulioanza kufanya nao mazungumzo basi tutawasajili lakini ikishindikana tuna vijana wengi wa U20,” alisema na kuongeza:

“Kadiri siku zinavyoenda mbele vijana wetu wanazidi kuimarika hivyo tutaendelea kuwatumia na watakuwa bora zaidi.”

Hata hivyo, benchi la ufundi la Mtibwa limeshauri kuiangalia upya safu yao ya ushambuliaji kwani alipata nafasi lakini ilishindwa namna ya kuzitumia vizuri kupata mabao.

Msembaji wa Mtibwa, Thobias Kifaru alisema Ligi Kuu imekuwa na ushindani mkali na kuwataka watu wasiibeze Yanga.

“Yanga iheshimiwe, uzembe ulifanyika kipindi cha kwanza wakatufunga lakini kipindi cha pili timu ilibadilika ila tatizo lipo kwenye umaliziaji wa nafasi tulizopata, hivyo makocha waliangalie hilo” alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live