Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliepewa "Thank you" Azam FC aibukia kwa "Wajeda"

Aziz Kader Ismail Aziz Kader

Mon, 19 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Siku chache tangu atemwe na Azam FC, kiungo Ismail Aziz Kader ametua kwa maafande wa JKT Tanzania iliyorejesha Ligi Kuu Bara kwa msimu ujao akiwa sambamba na Deusdedith Okoyo wakipewa mkataba wa kuitumikia timu hiyo kwa miaka miwili.

Mwanaspoti awali liliandika kwamba Okoyo anakuja Dar es Salaam kwa ajili ya kumalizana na JKT Tanzania na Ijumaa alivyofika tu alipewa mkataba huo na kusaini.

Upande wa Kader yeye baada ya kumalizana na Azam, aliitwa na mabosi wa JKT Tanzania na walikaa chini kisha akasaini mkataba wa miaka miwili.

Chanzo kimoja kutoka ndani ya JKT Tanzania kililiambia Mwanaspoti kwamba wanataka kuijenga timu yao kuhakikisha wakipanda wanakuwa kwenye ubora wa hali ya juu na kuleta ushindani.

"Hao tayari wameshasajiliwa na lengo ni kwenda kuongeza ushindani katika kikosi chetu, timu inatakiwa kuwa imara kwa sababu tunataka kuleta ushindani,"kilisema chanzo hicho.

Alipotafutwa kocha mkuu wa timu hiyo, Malale Hamsini alisema ameshakabidhi ripoti kwa viongozi wao na wanachosubili ni dirisha lifunguliwe tu.

"Maeneo yote matatu ambayo ni ulinzi, kiungo na ushambuliaji tutasajili lakini kwa sasa siwezi kusema, ila dirisha likifunguliwa tutasajili na mtawaona," alisema Malale.

JKT ilishuka Ligi Kuu msimu wa 2020/21 na sasa imerejea tena.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live