Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alieichapa Yanga kwa Mkapa ampa mbinu Gamondi

Pluijm 197 1024x640.png Hans Pluijm

Wed, 29 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa zamani wa Yanga Mholanzi, Hans van der Pluijm amesema ili kikosi hicho kipate matokeo mazuri ni lazima kicheze kwa tahadhari na kwa nidhamu kubwa kuanzia eneo la kujilinda hadi katika ushambuliaji.

Pluijm ambaye ndiye kocha aliyeipa ushindi pekee Yanga mbele ya Ahly kwenye hatua ya kwanza mtoano Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2014 katika uwanja wa Mkapa ikishinda 1-0 bao likifungwa na Nadir Haroub ‘Cannavaro’.

Plujim amesema “Yanga inacheza na timu nzuri Afrika lakini haipaswi kuwaogopa kwa sababu iko nyumbani na inahitaji pointi tatu baada ya mechi ya kwanza kupoteza, naamini inaweza kushinda endapo tu itazuia vizuri na kila nafasi itakayopata itaitumia vyema.”

Kocha huyo ameongeza kuwa Yanga inapaswa kutowapa nafasi wapinzani wao ya kuwashambulia kwa kuhakikisha inacheza kwa muunganiko mzuri kwani ina washambuliaji bora hivyo njia nzuri ya kuwazuia ni kucheza na kutowapa mianya ya kuwashambulia zaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live