Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliehitajika Simba aibukia Ihefu

Victorien Adebayor Deal.jpeg Kiungo Mshambuliaji,Victorien Adebayor

Mon, 15 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwandishi wa kujitegemea wa habari za michezo hasa masuala ya usajili kutoka nchini Ghana, Micky Jr amethibitisha kuwa klabu ya Ihefu (Singida Black Stars) imekamilisha usajili wa aliyekuwa winga wa US Gendamarie ya Niger na RS Berkane Victorien Adebayor ambaye aliwaniwa na Simba misimu miwili iliyopita.

Adebayor ambaye kipindi cha nyuma aliziingiza vitani Simba na Vigogo wa Morocco RS Berkane baada ya kunaswa na wa Morocco hao hakuwa na kiwango bora kabla ya kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu kwa majeraha kisha kusaini mkataba na Amazulu ambako nako hakutumikia mkataba huo mpaka sasa.

Ihefu imekuwa na kisu kikali kwenye soko la usajili ikipigana vikumbo na vilabu vikubwa vya nchini kama Simba na Yanga na vile vya kimataifa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live