Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliefeli Azam aahidi makubwa KMC, atatoboa?

Moallin Azam FC Abdihamid Moallin

Fri, 14 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Abdi Hamid Moallin ni kocha mpya ndani ya kikosi cha KMC chenye ngome yake pale Kinondoni.

Kocha huyo ambaye amewahi kuifundisha Azam FC amerejea kwa mara nyingine kwenye ardhi ya Bongo.

Safari hii atakuwa na KMC kuipambania ndani ya Ligi Kuu Bara msimu mpya ujao.KMCKMC haikuwa na mwendo mzuri ndani ya msimu wa 2022/23 ilipata nafasi ya kubaki ndani ya ligi kwa mchezo wa mtoano.

Kocha huyo amesema kuwa hiyo kwake ni fursa anaamini atafanya kazi kwa ushirikiano ili kupata matokeo chanya.

“Tunaamini kuwa utakuwa ni msimu mzuri na ligi ina ushindani mkubwa hivyo tutapambana na kufanya kazi kwa ushirikiano hii kwangu ni fursa nzuri,”.

Moallin alikuwa na kikosi cha Azam FC lakini akaondolewa baada ya kushindwa kuuridhisha uongozi wa Azam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live