Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alichokisema Banda baada ya majibu ya vipimo vya corona

99517 Pic+banda Alichokisema Banda baada ya majibu ya vipimo vya corona

Fri, 20 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaan. Beki wa kimataifa wa Tanzania, Abdi Banda amesema hana maambukizi ya virusi vya corona.

Banda anayecheza Highlands Park ya Afrika Kusini hana virusi hivyo ambavyo vimeleta taharuki duniani.

Awali, Banda alionekana na dalili ya ugonjwa huo, lakini majibu ya jana yamethibitisha yuko vizuri kiafya.

“Nilikuwa nikijihisi hivyo nikachukua hatua ya kufanyiwa vipimo, jambo jema majibu yametoka nipo salama,” alisema Banda.

Muda mfupi baada ya majibu alishukuru Watanzania waliokuwa pamoja naye katika kipindi alichokuwa akihisi ugonjwa huo.

Banda aliwataka Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga na maambukizi ya virusi hivyo vilivyotikisa dunia.

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement
Beki huyo mwenye uwezo wa kucheza nafasi zaidi ya moja uwanjani alikuwa mchezaji wa kwanza wa Tanzania kuhisiwa na virusi vya corona kabla ya kuthibitika yuko fiti.

Chanzo: mwananchi.co.tz