Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alichokifanya Ball Kid mechi ya Yanga vs CR Belouizdad ni ushujaa

Ball Kidszz Alichokifanya Ball Kid mechi ya Yanga vs CR Belouizdad ni ushujaa

Mon, 26 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuna mtoto juzi (Ball Kid) kwenye mechi ya Yanga baada ya bao la nne kuna tukio alilifanya ili kupoteza muda, kwangu naona tukio la kishujaa sana, alimpa mpira Kouassi Yao Yao kisha akachukua mwingine akautupa uwanjani, ni kama alimsignal Yao Yao kuwa usiufuate huo mpira, akaruka mabango akaingia uwanjani pembeni kuuchukua.

Tukio la Kijana kufanya hivyo mbele ya umati mkubwa bila kuhofia camera ilikuwa ni uthubutu mkubwa sana, Kisaikolojia alishajiandaa sana maana kumzuia Yao Yao asiufuate ule mpira na yeye kuufuata huku anatembea taratibu ilikuwa akili kubwa na ya ziada sana, huo ndio ukomavu linapokuja suala la maslahi ya Taifa.

Mwamuzi na Yao Yao pekee ndio waliogundua, Mwamuzi akaenda kumuonya Dogo lakini tayari alikuwa amewapotezea kama sekunde 40, kuna wakati kitu kimoja kuhusu mpira wa miguu wala sio mpira wa miguu! Mliliona hili tukio?

Binafsi limenivutia, maana kule Algeria fainali ya Yanga na USMA, mpaka Waandishi walikuwa wanatupa mipira uwanjani.

Nilikuwepo pale Algiers, Waandishi walikaa nyuma ya magoli yote mawili kisha Ball Kids walisambazwa kila upande wa uwanja, wakati Yanga wanashambulia sana kazi yao ilikuwa ni kutupa mipira uwanjani kuingilia mchezo, wakati wa kurusha mpira hali ilikuwa hivyo hivyo! Yes ndio mpira ulivyo Afrika, ni suala la uzalendo wakati mwingine hakuna namna.

Farhan Kihamu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live