Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ali Kamwe amtaja Namba 6 Young Africans

Kamwe Tena Ms.jpeg Ally Kamwe

Sat, 8 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Imeelezwa kuwa Kiungo Mkabaji kutoka nchini Ivory Coast Zougrana Mohamed anayehusishwa na Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans, tayari ametua nchini kumalizana na timu hiyo.

Kiungo anayetokea klabu ya Asec Mimosas, anatarajiwa kupewa jezi namba sita ambayo ilikuwa inatumiwa na aliyekuwa staa wa timu hiyo, Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’, aliyetimkia Azam FC.

Kwa mujibu wa habari kutoka Young Africans zinadai kuwa nyota huyo atakuwa sehemu ya wachezaji ambao wataingia kambini keshokutwa kujiandaa na msimu mpya wa 2023/24.

Habari hizo zimeeleza kuwa, siku yoyote kuanzia jana Ijumaa 9Julai 07) majira ya jioni walitarajia kumtambulisha mchezaji huyo pamoja na wengine ambao watawatumia katika msimu ujao.

Afisa Habari wa Young Africans, Ally Kamwe, amesema kila mchezaji ambaye wamepanga kumpa mkataba watamtangaza kupitia kurasa za mitandao ya kijamii za klabu hivyo, mashabiki wa Young Africans wanatakiwa kuwa wavumilivu.

Kamwe amesema kikosi chao kimerejea salama nchini kutokea Malawi ambapo walikuwa katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Nyasa Big Bullets ambao ulichezwa juzi Alhamis (Julai 06) mjini Lilongwe na kumalizika kwa suluhu.

Amesema wanashukuru Mungu wamerejea nchini salama baada ya kufanikiwa kuonyesha mchezo mzuri licha ya mchezaji wao Denis Nkane kupata majeraha yaliyotokana na kuumia baada ya kugongana na beki wa Nyassa Big Bullets.

“Hali ya Nkane inaendelea vizuri lakini kutokana na ushauri wa madaktari anatakiwa afanyiwe vipimo kwa umakini, tunamshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kutuma watu wake kuhakikisha mchezaji huyo anatibiwa na daktari wa Ofisi ya Rais na hilo limefanyika baada ya kutua nchini amepokelewa na maafisa hao,” amesema Kamwe.

Ameongeza kuwa baada ya kurejea nchini kazi kubwa watakayoifanya ni kutambulisha benchi lao la ufundi litakaloongozwa na Kocha Miguel Angel Gamondi ambaye tayari amewasili jijini Dar es salaam na wasaidizi wake.

“Ndani ya hizi siku mbili tumewaacha Wanayanga kuwa na muda nzuri wa kupendeza kununua jezi zao mpya, ndani ya saa 24 hizi pia tutaweka wazi ni kiasi gani tumeuza jezi, tutawaeleza kuwa tumeauza jezi ngapi na thamani yake.

“Baada ya hili ndiyo suala la benchi la ufundi halafu hapo tutaanza kutangaza silaha zetu na yule namba sita tayari yuko nchini, kinachosubiriwa ni kumtambulisha tu na Wanayanga kumfahamu,” amesema Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: